Thursday, 30 November 2017

RAILA ASEMA ATAFUATA KATIBA

Kiongozi wa muungano wa NASA Bwana Raila Odinga amesema kuwa muungano wake utafuata sheria za katiba kuwasilisha lalama zao za kuonyesha kuwa hawana imani na serikali ya Jubilee, Haya yanajiri baada ya Bwana Odinga kuapa kuwa ataapishwa mnamo Disemba 12. Aliyasema haya kwenye barabara ya Manyanja  jijini Nairobi.

Odinga pamoja na wafuasi wake wameapa kutomtambua Rais Uhuru Kenyatta kuwa rais wa kenya wakisema kuwa hakuchaguliwa kwa njia halali
Picha ya Kinara wa NASA Raila Odinga

Akizungumza na kituo cha CNN Odinga alisema kuwa yuko makini katika kudumisha katiba na utawala wa sheria hata baada ya kusema siku ambayo ataapishwa licha ya hatua hiyo kusemwa kuwa ni ukiukaji wa katiba. Odinga aliongeza kuwa yuko tayari kwa mazungumzo.

WHAT DOES IT TAKE TO BE A LANDLORD IN TOWN?

 By Sifuma N. Lilian In light of the recent demolitions that are happening in the capital, it is always good to ensure that you’re follo...