Saturday, 23 December 2017

WATU SABA WAFARI KATIKA AJALI YA BARABARA

Watu saba wameripotiwa kuaga dunia asubuhi ya leo( jumamosi,23 desemba) baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugongana na lori katika eneo la Sultan Hamud katika Kaunti ya Makueni.kwenye barabara ya Nairobi -Mombasa.
Image result for photo of the latest accident that has happen in makueni on 23 december 2017
Magari yaliohusika katika ajali

Saba hao walikumbana na mauti walipokuwa njiani wakielekea kwenye matanga. Kamishna wa kaunti ya Makueni Mohammed Maalim amedhibitisha ajali hiyo akielezea kuwa dereva wa gari hilo lililokuwa limebeba waombolezaji lilikuwa linajaribu kulipita gari lilipogongana na lori lililokuwa likielekea Nairobi kutoka Mombasa.

Takriban watu 180 wamepoteza maisha yao kutokana na ajali ya barabara tangu mwezi disemba ulipoanza huku sababu kuu za ajali hizo kutokea zikiwa kuendesha gari kwa kasi, uendeshaji gari wakati dereva amelewa na kadhalika
Siku ya Jumanne disemba 19 serikali kupitia halmashauri ya usalama barabarani NTSA ilitoa orodha mpya ya hatua zitakazochukuliwa dhidi ya madereva watakaovunja sheria hizo hii ikiwa njia moja wapo tu ya kupunguza ajali barabarani .

No comments:

Post a Comment

WHAT DOES IT TAKE TO BE A LANDLORD IN TOWN?

 By Sifuma N. Lilian In light of the recent demolitions that are happening in the capital, it is always good to ensure that you’re follo...