| Afisa wa NTSA akikagua gari barabarani |
Sherehe na shamrashamra za krismasi zikiwa zimewadia wengi hufunga safari ya kutoka mijini kuelekea vijijini ili kujiunga na jamii zao.
Mishemishe hizo zikiendelea wengi wa madereva wameweza kutahadharishwa dhidi ya kutofuata sheria za barabarani. Haya yanajiri siku chache tu baada ya taifa kushuhudia jinamizi la ajali ambapo takriban watu 150 waliangamia katika ajali za barabara huku swala hili likizua wasiwasi. Halmashauri ya kusimamia usalama barabarani NTSA ikitaja maeneo kama vile Salgaa,Sachang'wan,Migaa,Soysambu na Manyani kuwa maeneo hatari. Vilevile NTSA imewapeleka maafisa wake kwenye barabara kuu ili kuhakikisha kuwa sheria zote za barabara ili kupunguza ajali ambazo zinashuhudiwa kila uchao
No comments:
Post a Comment