Friday, 22 December 2017

KNUT YAPINGA MATOKEO YA KCSE

Image result for picture of wilson sossion
Katibu mkuu wa KNUT Wilson Sossion

Chama cha walimu nchini KNUT kinataka matokeo ya mwaka huu ya mtihani wa K.C.S.E kufutiliwa mbali na mtihani huo kusahihishwa upya. Katibu mkuu wa chama hicho Wilson Sossion amesema matokeo hayo yanatia hofu ikizingatiwa muda mchache uliotumiwa kusahihisha mtihani huo.

Sossion  ametaka baraza la mtihani nchini KNEC kushurutishwa kuonyesha karatasi za majibu na jinsi zilivyo sahihishwa. Katibu huyo vilevile ameibua wasiwasi kuhusu idadi ndogo ya wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga na vyuo vikuu mwakani akisema idadi hiyo ni ndogo na imewashusha wengi matumaini ya kupata nafasi katika vyuo vikuu nchini.

Shinikizo hizo zinajiri huku mwanaharakati Okiya Omtatah akiwasilisha kesi mahakamani kutaka matokeo ya K.C.S.E kutupiliwa mbali. Omtatah katika kesi hiyo ameitaka baraza la mitihani KNEC kawasilisha karatasi zote za majibu kuonyesha jinsi mitihani ilivyosahihishwa.

Kesi hiyo itasikizwa tarehe 24 Januari mwaka 2018. Kauli sawa na hiyo imetolewa na kinara wa upinzani Raila Odinga akitaka jopo maalum kuundwa ili kuchunguza ni kwa nini watahiniwa wengi walifeli

No comments:

Post a Comment

WHAT DOES IT TAKE TO BE A LANDLORD IN TOWN?

 By Sifuma N. Lilian In light of the recent demolitions that are happening in the capital, it is always good to ensure that you’re follo...