Friday, 22 December 2017

KNHCR YATOA RIPOTI YAKE KUHUSU UHAINI ULIOFANYIKA WAKATI WA UCHAGUZI

Kila baada ya uchaguzi mkuu nchini mambo tofauti hujitokeza, uchaguzi wa hivi majuzi wa Agost 8 na Oktoba 26 ukikumbwa na visa vya uhaini, wizi na uharibifu wa mali.

Uchaguzi huu uliweza kukuja na maafa mengi takriban visa 86 vya ukatili wa kijinsia vikiripotiwa katika jiji la Nairobi wakati na hata baada ya uchaguzi.

Kulinganana ripoti ya shirika la kutetea haki za kibinadamu Kenya National Commission on Human rights (KNHCR) inasemekana asilimia 62 ya visa hivi viliendelezwa na maafisa wa polisi huku asilimia 38 ikiendelezwa na raia. Ripoti hiyo pia inaonyesha kuwa watu 35 waliuawa kati ya mwezi Septemba na Oktoba. Ripoti hii inajiri baada ya shirika hilo awali kutoa ripoti nyingine ilioonyesha visa 57 vya watu waliouawa wakati wa uchaguzi mkuu.
Image result for picture of police harassment during the election period in kenya
Polisi wakiwakabili waandamanaji

Kati ya waliouawa ni watoto, wanawake wawili na wengine wakiwa wanaume kati ya umri wa miaka 18 na 50. Mwenyekiti wa KNHCR Kagwiria Mbogori alisema kuwa wahasiriwa wote waliaga kutokana na risasi isipokuwa wawili

No comments:

Post a Comment

WHAT DOES IT TAKE TO BE A LANDLORD IN TOWN?

 By Sifuma N. Lilian In light of the recent demolitions that are happening in the capital, it is always good to ensure that you’re follo...