Abiria wengi waliokuwa wanatarajia kusafiri usiku wa kuamkia siku ya Jumatatu wameathirika pakubwa kutokana na marufuku ya serikali na mamlaka ya usalama barabarani NTSA kusitisha usafiri wa usiku.Hatua hiyo imejiri kufuatia ajali mbaya iliyotokea eneo la migaa kaunti ya Narok ambapo watu 36 waliaga dunia siku ya Jumapili, huku ikichangia nauli kupanda mara dufu katika baadhi ya maeneo nchini.
Baadhi ya kampuni za mabasi za kubeba abiria wanaotoka Mombasa wakija jijini Nairobi zimeongeza nauli hadi shilingi elfu mbili (2000) kiwango ambacho ni cha juu sana ikilinganishwa na ile ya kawaida ambayo ni elfu moja(1000).Hali sawa na hiyo imeshuhudiwa katika vituo vya mabasi mjini kitale kaunti ya Trans-nzoia huku baadhi ya abiria wakilalamikia marufuku hiyo wakisema hatua hiyo imekuwa ya ghafla na ya kutokuwa na suluhu kwa tatizo la ajali barabarani
Mwenyekiti wa baraza la magavana Jospahat Nanok amesema ni sharti NTSA ishirikiane na halmashauri ya ujenzi barabara kuu ili kutafuta suluhu ya ajali hizo. Nanok vilevile amesema ni jambo la kusikitisha kwa wakenya wengi kuaga dunia kufuatia ajali zinazoweza kuepukika
No comments:
Post a Comment