Wednesday, 6 December 2017

MAPENDEKEZO YA ELIMU YAPINGWA

Mapendekezo ambayo yametolewa na serikali katika sekta ya elimu humu nchini imeibua hisia mseto na kupingwa vikali na walimu wakati wakiwa katika kongamano lililofanyika mjini mombasa kongamano ambalo liliwaleta pamoja zaidi ya walimu wakuu elimu 12,000
akiwahutubia huko mombasa katibu katika wizara ya elimu Dkt.Richard Belio Kipsang' alisema kuwa serikali imeweka mikakati ambayo itahakikisha elimu bila malipo kwa shule za upili inafanikishwa.

Image result for picha za kongamano la walimu wakuu mombasa
Kongamano la walimu mjini Mombasa

Hata hivyo swala la kuwa na mwalimu mkuu mmoja wa shule za msingi na upili zinazotumia ua moja liliweza kupingwa na baadhi ya wakuu hao huku wakitaja hatua hiyo kama itakayochangia kusambaratika kwa viwango vya elimu hapa nchini na hivyo kupendekeza kuwepo kwa mikakati maalum itakayowezesha ufanisi wa elimu bila malipo kwa shule za upili

Vilevile mpango wa usambazaji vitabu katika shule za msingi na upili zinatarajiwa kuanza mapema hapo mwakani huku takriban wanafunzi millioni tisa wakitarajiwa kunufaika na mpango huu. Wachapishaji wa vitabu humu nchini pia hawajakumbatia mabadiliko haya huku wakiwa na hofu ya kutochaguliwa kwa mashirika yao huku ya kiserekali yakipewa kipao mbele.

No comments:

Post a Comment

WHAT DOES IT TAKE TO BE A LANDLORD IN TOWN?

 By Sifuma N. Lilian In light of the recent demolitions that are happening in the capital, it is always good to ensure that you’re follo...