Thursday, 7 December 2017

SERIKALI YATANGAZA SIKU YA MWISHO YA KUFANYA MTIHANI WA KCSE

Taasisi ya mtaala nchini (KICD) siku ya Juma tano (06/12/2017) ilitangaza mwaka 2022 kuwa ya mwisho kwa mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne KCSE

Akiwahutubia walimu wakuu katika kongamano lililowaleta pamoja walimu wakuu, mkurungenzi wa mtaala wa elimu Julius Jwang alisema kuwa mtaala wa zamani wa 8-4-4 utamalizika katika miaka saba ijayo. Vile vile alisema kuwa mtaala huo utatekelezwa katika viwango tofauti na kuwa walimu wataelimishwa ili kuhakikisha unafaulu.


Image result for PHOTO OF WILSON SOSSION
Picha ya Katibu mkuu wa elimu Wilson Sossion na Waziri wa elimu Fred Matiang'i

Aidha alisema kuwa shughuli hiyo haijaharakishwa akiongezea kuwa mwaka 2019 watasonga hatua nyingine darasa la nne na la tano likianziwa huku darasa la sita likitarajiwa kufikiwa ifikapo mwaka 2020.

Hata hivyo walimu walitupilia mbali mtaala huo mpya wa elimu wakisema kenya haiko tayari . Wakizungumza kwenye kongamano la wakuu wa shule linaloendelea mjini mombasa, walimu hao wameitaka serikali kusitisha mpango wa kuzindua mtaala huo mwakani. Katbu mkuu wa chama cha walimu Wilson Sossion alisema mtaala huo haujafanyiwa majaribio ipasavyo na kwamba hauwezi kutekelezwa kwani huenda ukafeli

No comments:

Post a Comment

WHAT DOES IT TAKE TO BE A LANDLORD IN TOWN?

 By Sifuma N. Lilian In light of the recent demolitions that are happening in the capital, it is always good to ensure that you’re follo...