Tuesday, 22 May 2018

Shule Ya Msingi Ya Kapsaret Yafungwa


Mvua inayoendelea kunyesha nchini imekuwa karaha na si furaha tena kwa wakaazi maeneo mbalimbali nchini.
Nyingi za shule zimelazimika kufungwa sababu kuu zikitokana na mvua ambayo imesababisha vyoo shuleni kuzama,hali ambayo hairuhusu masomo kuendelea kama kawaida.

Idara ya afya hii leo imefunga shule ya msingi ya Kapsaret kwenye kaunti ya Uasin Gishu kwa muda usiojulikana baada ya kuzama kwa vyoo shuleni humo kufuatia mvua kubwa inayoendelea kunyesha eneo hilo.


No comments:

Post a Comment

WHAT DOES IT TAKE TO BE A LANDLORD IN TOWN?

 By Sifuma N. Lilian In light of the recent demolitions that are happening in the capital, it is always good to ensure that you’re follo...