Saturday, 23 December 2017

WATU SABA WAFARI KATIKA AJALI YA BARABARA

Watu saba wameripotiwa kuaga dunia asubuhi ya leo( jumamosi,23 desemba) baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugongana na lori katika eneo la Sultan Hamud katika Kaunti ya Makueni.kwenye barabara ya Nairobi -Mombasa.
Image result for photo of the latest accident that has happen in makueni on 23 december 2017
Magari yaliohusika katika ajali

Saba hao walikumbana na mauti walipokuwa njiani wakielekea kwenye matanga. Kamishna wa kaunti ya Makueni Mohammed Maalim amedhibitisha ajali hiyo akielezea kuwa dereva wa gari hilo lililokuwa limebeba waombolezaji lilikuwa linajaribu kulipita gari lilipogongana na lori lililokuwa likielekea Nairobi kutoka Mombasa.

Takriban watu 180 wamepoteza maisha yao kutokana na ajali ya barabara tangu mwezi disemba ulipoanza huku sababu kuu za ajali hizo kutokea zikiwa kuendesha gari kwa kasi, uendeshaji gari wakati dereva amelewa na kadhalika
Siku ya Jumanne disemba 19 serikali kupitia halmashauri ya usalama barabarani NTSA ilitoa orodha mpya ya hatua zitakazochukuliwa dhidi ya madereva watakaovunja sheria hizo hii ikiwa njia moja wapo tu ya kupunguza ajali barabarani .

NTSA YAHAKIKISHA SHERIA ZA BARABARANI ZINAFUATWA

Image result for picture of NTSA
Afisa wa NTSA akikagua gari barabarani

Sherehe na shamrashamra za krismasi zikiwa zimewadia wengi hufunga safari ya kutoka mijini kuelekea vijijini ili kujiunga na jamii zao.

Mishemishe hizo zikiendelea wengi wa madereva wameweza kutahadharishwa dhidi ya kutofuata sheria za barabarani. Haya yanajiri siku chache tu baada ya taifa kushuhudia jinamizi la ajali ambapo takriban watu 150 waliangamia katika ajali za barabara huku swala hili likizua wasiwasi. Halmashauri ya kusimamia usalama barabarani NTSA ikitaja maeneo kama vile Salgaa,Sachang'wan,Migaa,Soysambu na Manyani kuwa maeneo hatari. Vilevile NTSA imewapeleka maafisa wake kwenye barabara kuu ili kuhakikisha kuwa sheria zote za barabara ili kupunguza ajali ambazo zinashuhudiwa kila uchao

Friday, 22 December 2017

KNUT YAPINGA MATOKEO YA KCSE

Image result for picture of wilson sossion
Katibu mkuu wa KNUT Wilson Sossion

Chama cha walimu nchini KNUT kinataka matokeo ya mwaka huu ya mtihani wa K.C.S.E kufutiliwa mbali na mtihani huo kusahihishwa upya. Katibu mkuu wa chama hicho Wilson Sossion amesema matokeo hayo yanatia hofu ikizingatiwa muda mchache uliotumiwa kusahihisha mtihani huo.

Sossion  ametaka baraza la mtihani nchini KNEC kushurutishwa kuonyesha karatasi za majibu na jinsi zilivyo sahihishwa. Katibu huyo vilevile ameibua wasiwasi kuhusu idadi ndogo ya wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga na vyuo vikuu mwakani akisema idadi hiyo ni ndogo na imewashusha wengi matumaini ya kupata nafasi katika vyuo vikuu nchini.

Shinikizo hizo zinajiri huku mwanaharakati Okiya Omtatah akiwasilisha kesi mahakamani kutaka matokeo ya K.C.S.E kutupiliwa mbali. Omtatah katika kesi hiyo ameitaka baraza la mitihani KNEC kawasilisha karatasi zote za majibu kuonyesha jinsi mitihani ilivyosahihishwa.

Kesi hiyo itasikizwa tarehe 24 Januari mwaka 2018. Kauli sawa na hiyo imetolewa na kinara wa upinzani Raila Odinga akitaka jopo maalum kuundwa ili kuchunguza ni kwa nini watahiniwa wengi walifeli

KNHCR YATOA RIPOTI YAKE KUHUSU UHAINI ULIOFANYIKA WAKATI WA UCHAGUZI

Kila baada ya uchaguzi mkuu nchini mambo tofauti hujitokeza, uchaguzi wa hivi majuzi wa Agost 8 na Oktoba 26 ukikumbwa na visa vya uhaini, wizi na uharibifu wa mali.

Uchaguzi huu uliweza kukuja na maafa mengi takriban visa 86 vya ukatili wa kijinsia vikiripotiwa katika jiji la Nairobi wakati na hata baada ya uchaguzi.

Kulinganana ripoti ya shirika la kutetea haki za kibinadamu Kenya National Commission on Human rights (KNHCR) inasemekana asilimia 62 ya visa hivi viliendelezwa na maafisa wa polisi huku asilimia 38 ikiendelezwa na raia. Ripoti hiyo pia inaonyesha kuwa watu 35 waliuawa kati ya mwezi Septemba na Oktoba. Ripoti hii inajiri baada ya shirika hilo awali kutoa ripoti nyingine ilioonyesha visa 57 vya watu waliouawa wakati wa uchaguzi mkuu.
Image result for picture of police harassment during the election period in kenya
Polisi wakiwakabili waandamanaji

Kati ya waliouawa ni watoto, wanawake wawili na wengine wakiwa wanaume kati ya umri wa miaka 18 na 50. Mwenyekiti wa KNHCR Kagwiria Mbogori alisema kuwa wahasiriwa wote waliaga kutokana na risasi isipokuwa wawili

Thursday, 21 December 2017

IMANI TELEVISION: AYIRO, "SOMO LA UANASHERIA LIMEIDHINISHWA CHUONI M...

IMANI TELEVISION: AYIRO, "SOMO LA UANASHERIA LIMEIDHINISHWA CHUONI M...: Lango la shule ya uanasheria Kaimu naibu mkuu wa chuo kikuu cha Moi mjini Eldoret amekana madai kwamba chuo hicho hakijaidhinishwa k...

IMANI TELEVISION: WASICHANA WANG'AA TENA

IMANI TELEVISION: WASICHANA WANG'AA TENA: Wanafunzi wa kike wamegonga tena vichwa vya habari kwa kudhihirisha umahiri wao katika masomo na kuwashinda wenzao wa kiume mwaka huu kati...

Monday, 11 December 2017

Barabara mbovu katikati mwa mji wa kitale

MAHAKAMA KUTOA RIPOTI KUHUSU KUIDHINISHA USHINDI WA RAIS KENYATTA

Majaji wa mahakama ya juu siku ya leo (Jumatatu) wanatarajiwa kuelezea kikamilifu sababu zilizopelekea kuafikia uamuzi wa kuidhisha ushindi wa rais Uhuru Kenyatta kwenye uchaguzi wa Oktoba 26

Msajili wa mahakama alisema kuwa uamuzi utaanza kutolewa sa nane ikiongozwa na jaji mkuu David Maraga na naibu jaji mkuu Philomena Mwilu huku wakitarajiwa kuelezea ni kwa nini waliidhinisha ushindi wa rais Uhuru Kenyatta. Majaji wengine ambao watakuwepo ni Jaji Jackton Ojwang, Smokin Wanjala, Njoki Ndung'u na Isaac Lenaola

Image result for PHOTO OF PANEL OF JUDGES OF KENYA
Supreme Court Judges
Mahakama pia inatarajia kuelezea iwapo uchaguzi uliathirika ikizingatiwa kuwa maeneo bunge 25 hazikushiriki kwenye uchaguzi. Kesi mbili zilipelekwa mahakamani kupinga ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta katika marudio ya uchaguzi uliofanyika

Njonjo Mue na Khalef Khalifa walidai kuwa uchaguzi uliendashwa pasi na kufuata katiba na ilivyoagizwa na mahakama mnamo september 1. Mwanasiasa Harun Mwau naye alipeleka kesi mahakamani huku akidai kuwa tume ya IEBC iliendesha uchaguzi bila kufanya upya zoezi la uteuzi la majina ya wawaniaji urais kabla ya kuchapisha majina ya nane hao


Friday, 8 December 2017

NETANYAHU APPRECIATES TRUMP'S FOR HIS MOVE

Jerusalem Prime Minister Benjamin Netanyahu has send a message of appreciation to the US President Donald Trump regarding his statement on which he recognized Jerusalem as the capital city of Israel. Netanyahu through his twitter handle acknowledged the president's move as a brave move and termed it as a historic decision given that POTUS had received warnings from around the world claiming the move will bring a gap between Israel and Palestine

Image result for PHOTO OF BENJAMIN NETANYAHU
Photo of Israel Prime Minister Benjamin Netanyahu


However Donald Trump said that recognising Jerusalem as the capital city of Israel is in pursuit to bring peace between Israel and Palestine and further state he will move the US Embassy in Tel Aviv to Jerusalem

Thursday, 7 December 2017

SERIKALI YATANGAZA SIKU YA MWISHO YA KUFANYA MTIHANI WA KCSE

Taasisi ya mtaala nchini (KICD) siku ya Juma tano (06/12/2017) ilitangaza mwaka 2022 kuwa ya mwisho kwa mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne KCSE

Akiwahutubia walimu wakuu katika kongamano lililowaleta pamoja walimu wakuu, mkurungenzi wa mtaala wa elimu Julius Jwang alisema kuwa mtaala wa zamani wa 8-4-4 utamalizika katika miaka saba ijayo. Vile vile alisema kuwa mtaala huo utatekelezwa katika viwango tofauti na kuwa walimu wataelimishwa ili kuhakikisha unafaulu.


Image result for PHOTO OF WILSON SOSSION
Picha ya Katibu mkuu wa elimu Wilson Sossion na Waziri wa elimu Fred Matiang'i

Aidha alisema kuwa shughuli hiyo haijaharakishwa akiongezea kuwa mwaka 2019 watasonga hatua nyingine darasa la nne na la tano likianziwa huku darasa la sita likitarajiwa kufikiwa ifikapo mwaka 2020.

Hata hivyo walimu walitupilia mbali mtaala huo mpya wa elimu wakisema kenya haiko tayari . Wakizungumza kwenye kongamano la wakuu wa shule linaloendelea mjini mombasa, walimu hao wameitaka serikali kusitisha mpango wa kuzindua mtaala huo mwakani. Katbu mkuu wa chama cha walimu Wilson Sossion alisema mtaala huo haujafanyiwa majaribio ipasavyo na kwamba hauwezi kutekelezwa kwani huenda ukafeli

Wednesday, 6 December 2017

MAPENDEKEZO YA ELIMU YAPINGWA

Mapendekezo ambayo yametolewa na serikali katika sekta ya elimu humu nchini imeibua hisia mseto na kupingwa vikali na walimu wakati wakiwa katika kongamano lililofanyika mjini mombasa kongamano ambalo liliwaleta pamoja zaidi ya walimu wakuu elimu 12,000
akiwahutubia huko mombasa katibu katika wizara ya elimu Dkt.Richard Belio Kipsang' alisema kuwa serikali imeweka mikakati ambayo itahakikisha elimu bila malipo kwa shule za upili inafanikishwa.

Image result for picha za kongamano la walimu wakuu mombasa
Kongamano la walimu mjini Mombasa

Hata hivyo swala la kuwa na mwalimu mkuu mmoja wa shule za msingi na upili zinazotumia ua moja liliweza kupingwa na baadhi ya wakuu hao huku wakitaja hatua hiyo kama itakayochangia kusambaratika kwa viwango vya elimu hapa nchini na hivyo kupendekeza kuwepo kwa mikakati maalum itakayowezesha ufanisi wa elimu bila malipo kwa shule za upili

Vilevile mpango wa usambazaji vitabu katika shule za msingi na upili zinatarajiwa kuanza mapema hapo mwakani huku takriban wanafunzi millioni tisa wakitarajiwa kunufaika na mpango huu. Wachapishaji wa vitabu humu nchini pia hawajakumbatia mabadiliko haya huku wakiwa na hofu ya kutochaguliwa kwa mashirika yao huku ya kiserekali yakipewa kipao mbele.

WHAT DOES IT TAKE TO BE A LANDLORD IN TOWN?

 By Sifuma N. Lilian In light of the recent demolitions that are happening in the capital, it is always good to ensure that you’re follo...